A Closer Walk
Encourage One Another Daily - As Long As It Is Called Today! (Hebrews 3:13)

Home Today Archive Salvation About Resources Add Name
Reading Plans | Verses | Forums | Support | Spanish Devotionals
Book Store  |  Translations  Africa Ministry  |  Stacey Blog | Podcast | NEW!! Facebook !!!

 


A Closer Walk - Volume 1 Archive

English Message | Spanish Message

Kila Mara Tafuta Ushauri Wake

Musa alipokaribia kufa, alipitisha uongozi wa Israeli kwa Yoshua. Mungu alitoa thibitisho yake kwa Joshua kwa maagizo; “uwe hodari tu na ushujuaa mwingi, aungalilie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako” (Yoshua 1:7).
Mwanzoni, Yoshua aliutafuta ushauri wa Mungu kwa kila hatua aliyochukuwa. Yoshua alipata mwelekeo wa kuvuka mto wa Yordani (Yoshua 3), kuujenga ukumbusho wa milele (Yoshua 4), kulifanya upya tena agano la tohara (Yoshua 5) na kuutumwaa mji uliofungwa wa Yericho (Yoshua 6) Kwa haya yote Yoshua alisikiliza na Kutii; “Basi Bwana alikuwa pamoja na Yoshua, sifa zake zikaenea katika nchi ile yote”. (Yoshua 6:27).
Hata hivyo, baada ya ufanisi wa kimiujiza kule Yeriko – baaba ya Yoshua kushuhudia kuta za mji zikianguka kwa sauti ya tarumbeta na kelele – tumaini la Yoshua lilianza kukua. Ilipokuwa wakati wa kushambulia mji mdogo wa Ai, Yoshua alitegemea nguvu zake mwenyewe na ushauri wa watu badala ya kumtafuta Mungu.
Yoshua 7:3-4
“Waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai, usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu. Basi watu wakaendahuko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu wa Ai.”
Kushambulia mji wa Ai ilikuwa hatua isiyofaa. Likuwa ni mji mdogo na jeshi la isarael lilikuwa shupavu, na Mungu alikuwa tayari ametoa maagizo ya kushambulia nchi yote na hakikisho la ushindi katika vita: “kila mahalizitakapopakanyaga nyayo za Mungu yenu, nimewapa ninyi… Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako” (Yoshua 1:3,5). Lakini, bila Yoshua kuujua; kulikuwa na dhambi katika kambi yako – vita vya kiroho ambavyo vingezuia ushindi wowote asili “Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao” (Yoshua 7:12). Hakukisho letu la ushindi kila mara watokea kwa kutembea na Mungu na kwa nguvu Zake.
Ni wakati gani mwisho tulipontafuta na kumpokea ushauri kutoka kwa Mungu? Kama imekuwa zamani kuliko wakati ilichukuwa kuchukuwa hatua yetu ya mwisho, tutakuwa tunajaribu kupigana vita tusivyoshinda. Tusijaribu kudhania tunajua mpango maalum wa Mungu bila kuuliza mwelekezo maalum. Kwa sababu alisema, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi” (Mathayo 28:19), haimaanisha tunaweza kuthubutu katika taratibu Yake au wasaa Wake; “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yohana 15:5).
Mungu atatuonyesha njia, lakini ni lazima tuukize ushauri Wake; “Nememweka BWANA mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa” (Zaburi 16:8). Vita vyetu hatushindi kwa sababu ya nguvu zetu au unyonge wa adui.Tunashinda tunapomruhusu Mungu kutushauri katika kila hatua. Haijalishi aumuzi wetu uonekanavyo usiofaa, wacha tukawe na hakika kutembea katika nguvu Yake na kila mara tafuta ushauri Wake.
Kuwa Na Siku Njema!
Steve Troxel
God's Daily Word Ministries