|
A Closer Walk - Volume 1 Archive |
|
English Message | Spanish Message |
|
Ili Ulimwengu Ujue |
|
|
| Katika ujumbe, “Nia ya kristo” tulizingatia mwito wetu wa kutembea kulingana na maisha mapya tuliyopewa. Tuliangalia baadaye tabia kadhaa za maisha ya Yesu kama mfano wetu halisi wa kufuata. Tuliona kutamani kwake kutumika na kumtukuza Baba, na pengine changamoto kubwa maishani mwa Yesu ilikuwa uwezo wake kusamehe; “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Luka 23:34). |
|
| Mwendo wa Mkirsto ni hali ya mageuzi ya maisha kwa mfano wa Yesu. Hali hii inaendelea kutuleta karibu na Mungu na kuonyesha dhairi ujumbe wa injili duniani. Hakuna uonyesho wazi wa moyo uliogeuzwa na upendo halisi kwa kristo kuliko tunaposamehe waliotukosea. Ukweli kwamba jambo hili ni ngumu linafanya msamaha kuwa nuru katika ulimwengu wa giza na unaokufa. Umoja upatikanao kupitia msamaha unafanya wale walio ulimwenguni kusongea karibu na kristo. |
|
| Yohana 17: 23 |
| “Ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.” |
|
| Kukamilika katika umoja si mwito wa kuzima ukweli halisi wa injili, lakini ni mwito wazi wa kuweka mbali ugomvi wa vitu vidogo vidogo na kutupilia mbali wivu wote, husuda, na mojawapo ya maovu makubwa yajulikanayo na mwanadamu....Kiburi! Kiburi kinawafanya watu wengi kutengwa na Mungu na uhusiano mwingi unasambaratika kwa ukosefu wa msamaha kuliko dhambi zingine. |
|
| Kuendelea kusamehe kunadhihirisha injili kwa sababu kunatuhitaji sisi kwa uaminivu kuyatazama majivuno yetu, kuweka matumaini yetu kwa Mungu, na kutembea kwa unyenyekevu sana. Kusamehe si kitu tunachofanya kwa nguvu zetu wenyewe. Tunapo “jeruhiwa,” kutendewa visivyo haki na kutoeleweka, kiburi chetu kinataka vitu viwe “hata”- kumhitaji mtu mwingine kukiri, kutubu, na kuinama kubusu miguu YETU. Msamaha wa kweli kwa wengine unatuleta nyuma kwa msalaba ambapo lazima tukiri uupotevu wa moyo wetu, tukubali mahitaji yetu ya msamaha wake, na, mara nyingine, tujiondoe wanyewe kwa kiti cha enzi. |
|
| Kuendelea kusamehe kunahitaji kila siku kusulubisha miili yetu, utu uliojaa kiburi, na kujitoa kwa uongozi wa Roho mtakatifu, na tumaini lote kwa Baba yetu wa mbinguni kuendeleza hali ambayo ameianzisha katika maisha yetu na kijumla kufanya kazi kwa maisha ya wengine (Kadiri ya ukamilifu wa wakati wake). Haya maisha ambayo bila shaka yanaangaza na kuufanya ulimwengu kujua. |
|
| Wacha tuchukuwe mtazamo mpya wa kukosa kusamehe na kuamua mara na kabisa kumwachia Mungu. Wacha tumtukuze Baba yetu na kuwa mfano hai wa Injili - wacha tuishi kwa umoja kupitia upendo na msamaha....ili ulimwengu ujue! |
|
| Kuwa Na Siku Njema! |
|
| Steve Troxel |
| God's Daily Word Ministries |