A Closer Walk
Encourage One Another Daily - As Long As It Is Called Today! (Hebrews 3:13)

Home Today Archive Salvation About Resources Add Name
Reading Plans | Verses | Forums | Support | Spanish Devotionals
Book Store  |  Translations  Africa Ministry  |  Stacey Blog | Podcast | NEW!! Facebook !!!

 


A Closer Walk - Volume 1 Archive

English Message | Spanish Message

Dhambi Ya Ujeuri.

Kwenye ujumbe “mpe yeye Utukufu wote” tulizingatia vile Yusufu alitambua uweza wake wa kufasiri ndoto uliwezakana tu kwa neema ya Mungu; “Mungu atampa Farao majibu ya amani” (Mwanzo 41:16). Tulikumbushwa pia kuhusu maneno ya Paulo kwa Wakorintho, “wajisifia nini kana kwamba hukupokea?” (1 Wakorintho 4:7), na yale ya Yesu, “maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yohana 15:5). Kumpa Mungu utukufu wote kunadhihirisha kujifahamu sisi ni nani kwa Kristo na, la muhimu sana, yeye ni nani kwetu!
Kama tunavyoona wingi wa dhambi katika dunia leo, ambazo zinawaletea maumivu wengine, tunapaswa kukumbushwa kwamba dhambi zote chanzo chake ni kiburi na kukosa unyenyekevu - hadi ujeuri, kujiinua wenyewe tunapojiwazia wenyewe na uweza wetu juu zaidi kuliko inavyopaswa; na mwishowe, kujaribu kujiweka juu ya Mungu.
Yakobo aliandika juu ya ujeuri huu aliposema “msisingiziane” (Yakobo 4:11). Alisema tunapokuwa wabishi visivyohaki kwa wenzetu si tu sheria ya upendo wa Mungu hatutii, bali hakika tunaidhihaki sheria ya Mungu na kuketi kuihukumu sheria – na kuna hakimu mmoja tu! (Yakobo 4:11-12). kutotii kimakusudi kunajumuisha kujienua wenyewe hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu na kuhukumu ambako kwa ukweli wake kunatekelezwa katika maisha yetu. Hiki ni kiburi kikubwa!
Isaya 14:13 – 15
“Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka Mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu, Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; mpaka pande za mwisho za shimo.”
Maneno haya yanamlenga shetani, ama mfalme wa ulimwengu wakati wa Isaya. Kwa vyovyote vile, inatueleza wazi ulivyo moyo wa kiburi vile vile matokeo ya mwisho ya moyo kama huo. Isaya anatuonya sote juu ya hatari ya kujaribu kujiiinua ili kufikia kiwango cha Mungu. Hata hivyo, kujaribu huku ndiko kulisababisha kushushwa kwa mwanadamu kutoka Bustani ya Edeni; “siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu” (Mwanzo 3:5).
Lazima twendelee kupeleleza moyo wetu na kwa ujasiri kukata sehemu zo zote za kiburi kabla kuambukiza na kuenea kwa utu wote. Tunaweza kujiondoa kwa kiburi chote wenyewe? Tunaweza kukomesha dhambi zote? Siamini eti tunaweza! Lakini ninajua kwamba siku tutakayomwona Yeye uso kwa uso, tutakuwa tumegeuzwa kabisa, tumetukuza kabisa, na kuweza kumsifu Yeye milele yote. Hadi siku atakayotuita nyumbani, lazima twendelee kusema, “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua” (Yohana 3:30). Mpaka siku hiyo, hatuna budi kupigana na dhambi ya ujeuri.
Kuwa Na Siku Njema!
Steve Troxel
God's Daily Word Ministries